Katika maisha mawazo ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu, lakini hata hivyo matumizi ya akili lazima yawekewe mipaka na isiwe ni kitu cha kawaida ubongo kuruhusiwa kwenda mwendo mkali kulingana na uwezo wake.
Waundaji wa mashine, kwa mfano, wakati wanatengeneza injini waliweka mwendo kasi wa kiwango cha juu, hata hivyo huonya kuwa si kila wakati mwendesha chombo cha moto anaruhusiwa kutumia ‘spidi’ zote zilizomo ndani ya mashine yake.
Hali hiyo ndiyo inayojitokeza katika uwezo wa ubongo katika kufikiri na kupata majibu ya kina ya nini kilichopo na kitakachotokea. Ni ukweli ulio wazi kwamba ubongo ni mashine kubwa yenye uwezo wa ajabu usioelezeka.
Watu wengi waliofanikiwa na wanaotaka kufanikiwa ni wale ambao wanajua namna ya kuutumia ubongo katika kupanga maisha
Lakini pamoja na umuhimu wa mwanadamu kutumia akili yake kupata majibu ya hisia, maono, mazingira na vitu anavyokutana navyo maishani, kuna wakati umuhimu huo hukosa maana na maonyo ya kuwa na udhibiti kasi ya fikra yanachukua nafasi.
Haijalishi mhusika ana uwezo wa kiasi gani ndani ya akili yake! Kumbuka pia onyo la dereva kutumia mwendo kasi kila anapowasha gari lake, halafu linganisha na akili yako au ya mwanadamu unayemtazama utagundua kuwa kithibiti mwendo kinahitajika hata katika mawazo.
Hebu chukua jukumu la kuutazama ulimwengu huu tulio nao na uangalie uozo wa wanadamu katika kujiheshimu, kisha ujiulize hivi kuna mwanaume au mwanamke ambaye anaishi bila kumsaliti mpenzi wake? Baada ya swali
Wakati unasubiri majibu endelea kuweka viashiria kichwani mwako kwa kumfikiria mkeo anayemhudumia bosi chai huko ofisini au Muuguzi anayefanya kazi chumba kimoja na Daktari usiku au askari polisi aliyeolewa anayekesha lindoni na bachela, kisha subiri majibu kutoka kwenye ubongo wako!
Bila shaka kwa mchakato huo mfupi tu majibu ya haraka yatakayokuja ni hakuna asiyesalitiwa. Isipokuwa kuna kuuficha ukweli. Sasa kwa majibu hayo ya akili mkeo unampenda nini wakati unafahamu kuwa anatoa penzi kwa wanaume wengine
Thamani ya ndoa na umuhimu wako unatoka wapi, tuseme hupati uchungu pale unapohisi unaibiwa mumeo?
Hapa ndipo penye kiini cha somo letu kwamba, kuna wakati tunaruhusu mawazo yetu yakimbie mwendo kasi kwenye njia yenye mabonde na kona na wengi wetu tumeharibu ndoa zetu na wengine tumeachana na wapenzi wetu kwa ujinga wa kutokuzuia kasi ya akili zetu.
Inashangaza kusikia na kuona kuna baadhi ya wanandoa wanaishi kwa kupelelezana kila siku
Hivi tulishawahi kujiuliza kuwa tunautumia ubongo wetu vibaya kutafuta ufumbuzi wa mambo ya kipuuzi!? Tunawafuatilia wake zetu maofisini kwao ili iweje? Hatuaminiani kwa nini wakati tumeoana, je mapenzi yana faida gani ndani ya usaliti na kujua kuwa sio wewe peke yako unayefaidi tunda la mkeo au mumeo.
Wakati nikitafakari kuhusu mada hii kaka mmoja aliniambia kuwa amempata mchumba ambaye ni mzuri
Binafsi sikufikiria
Maana haiwezi kuwa busara kwa mtu aliyemfuma mkewe na mwanaume mwingine atumie akili kujua ilikuwaje mpaka kukawepo makubaliano au msukumo upi ulimvuta mkewe kuutoa utu wake kwa mwanaume mwingine?
Inapofikia hatua hiyo umuhimu wa kulegeza mwendo wa akili kwa kusema sijui na sina haja ya kujua ilikuwaje, hata
Hii ndiyo siri ya usalama wa ndoa na uhusiano wa mapenzi ndani ya hofu ya usaliti. Ukiona mawazo yanakuja kutaka kutoa jibu la kuchelewa kwa mumeo kurudi huku dondoo za kuwepo kwa msichana mwingine kazini kwake zikichipuka, yatupilie mbali mawazo hayo. NDOA MAANA YAKE NI KUAMINIANA. UKIONDOA UAMINIFU HAKUNA NDOA!
No comments:
Post a Comment