MPENZI msomaji wa safu hii ya Hakunaga kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo sikuweza kukuletea mfululizo wa safu hii pendwa lakini hakijaharibika kitu hebu tuendelee kuzungumza lugha zetu za kimahaba na kimahusiano yanayojenga.
Wiki hii kama nilivyowaahidi awali kuwa tutaona njia kadhaa wanazoweza kuzitumia wanawake kuwa sumaku kwa wanaume wao.
Nimekuwa nikipa simu nyingi kutoka kwa akina dada ambao wamejaribu kuonesha hisia zao wazo kuwa licha ya kuumbika vizuri lakini hawajabahatika kuwa na wapenzi huku wengine wakisema kuwa hata kama wametongozwa lakini hawadumu katika mahusiano jambo ambalo nimeona leo nilitolee ufafanuzi na kukufundisheni.
1. Mwanamke jipende mwenyewe
Mwanamke ni lazima ujipende na kujiamini na ukigundua kuwa hisia zako zaapenzi zimejikita kwa huyo mwanaume ambaye hisia zako zinaamini kuwa ni yule ambaye umewahi kumuwaza kuwa ungependa kuwa nae basi usieleze kwanza uongo maana akija gundua weeeeee……noma.
Hapa niweke wazi kuwa ni muhimu mwanamke au mwanaume, kwa pamoja tujue kuwa tofauti yetu na mbuzi siyo miguu au manyoya bali kitu kingine kikubwa zaidi. Kitu hikikikubwa ndicho sisi – sisi ni jinsi tunavyofikiri ambapo kwa kufikiri kwetu tunakuwa kama tulivyo ambao ndiyo sisi wenyewe.
2. Jifunze namna ya kuzuga
Sisemi jifunze namna ya kudanganya bali ‘’kuzuga’’ naamini naeleweka vema ambapo wanawake wengi wenye kujua kuzuga wamekwa sumaku kubwa kwa wapenzi wao ama kwa wabnaume wanaowahitaji.
Wanawake wenye ujuzi wa kuzuga wamekuwa wakifanikiwa kuwanasa wanaume wengi kutokana na ujuzi wa kutumia viungo vyao walivyop[ewa na Mungu huku baadhi wakitumia macho yao kwa kuangaliana mara kwa mara na wanaume wanaovutiwa huku baadhi wakitumia midomo yao kuilamba kana kwamba anasawazisha mafuta katika midomo hiyo.
Mbinu hii inawapagawisha wanaume wengi ambao hujikuta akikuuluza jina ama moja kwa moja akakusogelea na kukusabahi na kujitambulisha ama kuomba namba yako ya simu, si unajua utandawazi umewapotezea wanaume wengi ujasiri wa kutongoza zaidi atakupigia simu, si mnajua wengi tunatongozana kupitia simu…si vibaya ingawa hamu inapotea kidogo.
3. Panga ratiba ya kutoka, ‘’siyo kusaka mabuzi’’
Wanawake wengine wamekuwa wakilaumu kuwa hawatongozwi na wanashindwa kuwadaka wanaume wanaowataka kimapenzi huku wao wenyewe wakiwa tatizo. Wengi hushinda nyumbani kama watoto wa Mfalme jambo ambalo wengine wamejikuta wakizeeka na kuanza kukumbuka hata kwa kulazimisha kuwa walau nwapate watoto.
Hali hii mwanamke utaiepuka endapo utakuwa na walau na ratiba zako nzuri hata kama haupendi kwenda Disko au ni geti kali basi hata week end uwe na ratiba ya kutembea ufukweni au mahala ambako unajua kuna watu wanajichanganya kidogo majira ya jioni na ahapa sizungumzii kuwa unaenda kutafuta soko bali kama unajiamini kuwa unamvuto naamini uchaguzi wako utakuwa mgumu kwasababau wengi watatamani kuwa nawe, si unaushawishi banaaaa…
4. Kosoa kwa hekima
Mbinu hii itawasaidia sana wanawake ambao wapo tayari kwenye ndoa na mahusiano ya kawaida ambapo kuna mahala wanawake wanajisahau na kuwatamkia wanaume wao maneno yasiyo na hekima, kwa mfano utamsikia mwanamke anamwambia mwanaume wake kuwa ‘’wanaume wenzako wanajenga, wewe kila siku ahadi tu’’ kauli kama hii ni kosa na kasoro kubwa.
Ukiachiliambali kwamba hiyo ni lawama, lakini kauli kama hiyo inajenga hisia kwa mwenzako kuwa mwanamke huyu kumbe anapenda kuwa na wanaume kama hao hivyo wanaume wengi hawapendi kushauriwa bila hekima na kudhani kuwa wanawake hao wanaodhani wanaume wao hao siyo wa maana hivyo mwanamke ukitumia maneno yasiyo na hekima huwezi kuwa sumaku kwa mwanamume wako.
Kwa leo tuishie hapa wiki ijayo na kuendelea nitakuletea mfululizo wa tofauti zetu yaani mwanamke na mwanaume na ujua kuwa kutentewa vizuri na mpenzi wako ni haki yako au la na hapo tutaelezana madogomadogo yafukuzayo wapenzi.
No comments:
Post a Comment